1 Machi 2019 - 10:51
 Urusi yapinga udhalimu wa Marekani dhidi ya Venezuela

Urusi na China zimepiga kura ya turufu dhidi ya azimio la Marekani katika baraza la Usalama la Umoja wa mataifa katika suala la mzozo wa Venezuela

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Urusi na China zimepiga kura ya turufu dhidi ya azimio la Marekani katika baraza la Usalama la Umoja wa mataifa katika suala la mzozo wa Venezuela , lakini mswada mbadala uliopendekezwa na Urusi pia haukupata kura za kutosha. Kushindwa kuchukua hatua katika miswada hiyo miwili kumeweka wazi mgawanyiko miongoni mwa mataifa yenye nguvu kuhusiana na hali nchini Venezuela , ambayo imetumbukia katika mzozo wa kisiasa unaochochewa na Marekani na vibaraka wake pamoja na kuporomoka kwa uchumi. Mswada uliopendekezwa na marekani unalenga kuingusha serikali halali ya rais Madulo, lakini Urusi na China zilizuwia mswada huo kwa kura ya turufu. Msawada wa Urusi , ambao unahimiza kutatuliwa kwa mzozo huo kwa njia ya amani na kusisitiza kwamba misaada yote ya kiutu ikubaliwe na serikali ya Maduro, ulipata kura nne tu za Urusi, China , Afrika kusini na Guinea ya Ikweta.

Mwisho wa habari / 291